9 Septemba 2025 - 14:05
Uteuzi wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt(a.s) kwa amri ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Khamenei; Amemteua Hujjatul-Islam wal-Muslimin Ramezani kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt(as) kwa muhula mwingine tena.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amemteua Hujjatul-Islam wal-Muslimin Ramezani kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (as) kwa muhula mwingine.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Akhtari, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (a.s), katika barua aliyoandika kwa Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, aliwasilisha ripoti kuhusu matokeo ya upigaji kura ya Baraza Kuu kuhusu watu waliopendekezwa kwa wadhifa wa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo.

Kwa kuwa Bwana Ramezani alipata kura nyingi, Kiongozi wa Mapinduzi alimteua rasmi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (a.s).

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha